KRC Genk Ya Samatta Inapumilia Mirija

Club ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta inaendelea kusuasua katika kutetea Ubingwa wake wa Ligi Kuu Ubelgiji kwa kuendelea kupoteza michezo.
Genk leo wakiwa wenyeji wa Sint-Truiden na wamepoteza nyumbani kwao kwa kufungwa magoli 2-1, Genk ndio walikuw wa kwanza kupata goli kupitia Mbwana Samatta dakik ya 9.
Mambo yalianza kubadilika dakika ya 18 Yoli alipofunga goli la kusawazisha kwa Saint Truiden, ushindi wa Truiden ukathibitishwa na Suzuki dakika ya 41 baada ya kufunga goli la ushindi, huu ni mchezo wa 7 kwa Genk kupoteza mchezo huu, Samatta akifunga goli lake la saba msimu huu katika Ligi Kuu.


EmoticonEmoticon