Kuhusu Ndoa Na Kuoa Mke Wa Pili, Alikiba Afunguka

Alikiba amehojiwa kwenye kipindi cha Leo tena ya Clouds FM ambapo ameulizwa kuhusu ndoa yake na kama angependa kuja kuoa mke wa pili hivi karibuni baada ya yeye kusema kuwa mke wake Amina kwa sasa yupo Mombasa Kenya.

Kwenye mahojiano hayo kuhusu ndoa yake Alikiba amesema kuwa, “Hakuna ndoa isiyokuwa na migogoro na ni vitu vya kawaida na sipendi kuongelea hilo, mimi sijawahi kulia kwenye mapenzi lakini nimewahi kuexperience maumivu lakini maumivu yangu hayawezi kufanana na ya kwako”.

Alikiba alipoulizwa kuhusu kuoa mke wake alijibu, ”Kwanini nishindwe, mkisikia nimeoa jua nimeamua mke wa pili mke wa tutu mke wa nne”


EmoticonEmoticon