Kwa Mara Nyingine Burna Boy Apigwa Nje Na South Africa

Burna Boy ameondolewa kwenye orodha ya watumbuizaji wa tamasha la Afropunk linalotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu Jijini Johannesburg Afrika Kusini.

Waandaaji wa tamasha hilo wametangaza rasmi siku ya Ijumaa kupitia twitter kuwa msanii huyo wa Nigeria ameondolewa.
Kwa mujibu wa maelezo yao wamesema huu sio muda sahihi kwa yeye kuja na kutumbuiza. Na walimaliza kwa kuomba radhi.

Hili ni tamasha la pili kwa Burna Boy kuondolewa nchini Afrika Kusini, mwezi uliopita aliondolewa kwenye tamasha la Africa Unite kufuatia kauli yake juu ya sakata la ubaguzi wa wageni (Xenophobia) miezi michache iliyopita.


EmoticonEmoticon