Mabaki Ya Ndege Iliyopotea Yaonekana

Maafisa wa Chile wanasema kwamba wamezuia mabaki yanayoaminika kutoka katika ndege ya kijeshi iliotoweka siku ya Jumatatu.
Wanasema kwamba mabaki hayo yalipatikana yakiolea kilomita 30 kutoka eneo ambalo ndege ya wanahewa wa Chile aina ya C-130 Hercules inayobeba mizigo ilikuwa na mawasiliano ya mwisho.
Vifusi hivyo vilipatikana katika maji yanayojulikana kama mkondo wa Drake.
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji wa kusini wa Chile wa Punta Arenas ikielekea katika kambi ya kijeshi ya Antarctica ambapo rais wa taifa hilo Eduardo Frei Montalva alikuwa.
Vifusi hivyo huenda vinatoka kutoka tangi la mafuta la ndege hiyo , kulingana na kamanda wa jeshi la wanahewa Eduardo Mosqueira ambaye alikuwa akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano.
Bwana Mosqueira alisema kwamba jeshi la wanahewa litafanya uchunguzi kubaini iwapo mabaki hayo yalikuwa ni yale ya ndege hiyo.
Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa kumi na mbili za jioni siku ya Jumatatu muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji wa Punta Arenas.
Jeshi la anahewa wa Chile lilitoa ramani ya njia iliofuata ndege hiyo na muda wake kwamba ilitarajia kutua mwendo wa saa moja na dakika 17 siku ya JUmatatu katika kambi hiyo ya Eduardo Frei Montalva.
Usakaji wa angani na baharini tayari umeanzishwa muda mfupi baada ya ndege hiyo kutoweka.
Argentina, Brazil, Uingereza na Uruguay zimetuma ndege kusaidia katika utafutaji wa ndege hiyo katika maji hayo ya barafu huku Marekani na Israel zikitoa picha za setlaiti.
Credit:bbc


EmoticonEmoticon