Maghorofa 10,000 Ni Hatari Kwa Maisha Ya Watu Kenya

Serikali nchini Kenya, imetahadharisha kuwa maghorofa zaidi ya 10,000 hayastahili watu kuishi kwa kuwa yanaweza kuanguka.
Ndani ya miezi michache iliyopita, watu zaidi ya mia wamefariki baada ya majengo ya gorofa waliyokuwamo kuanguka nchini humo, hususani katika jiji la Nairobi.
Kuporomoka majengo si jambo geni katika maeneo mengi barani Afrika.
Serikali ya Kenya imedai kuwa inachukua hatua lakini wakosoaji wake wanasema kuwa hakuna kinachoendelea na majengo ambayo yameorodheshwa ili yabomolewe bado watu wanaishi ndani yake. Mwandishi wa BBC Francis Ontomwa amefuatilia suala hilo na hii ni taarifa yake.

BY BBC


EmoticonEmoticon