Manchester City Wawaonya Arsenal Juu Ya Mikel Arteta

Manchester City wamekerwa na hatua ya Arsenali ya kumfuatilia kocha wao msaidizi Mikel Arteta na wameionya klabu hiyo kuwa itawabidi watoe donge nono ili wamnyakue kocha huyo.
Aidha, Arteta anatarajiwa kukutana na kiongozi mkuu wa Arsenal Josh Kroenke kwa ajili ya kufanya usajili wa tatu na wa mwisho huku akikaribia kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Unai Emery aliyetimuliwa mwezi uliopita.
Hata hivyo, Arteta yuko tayari kuacha wadhfa wake na kuchukua hatamu kama kocha wa Arsenali. 
Mzaliwa huyo wa Uhispaia ambaye hapo awali alichezea Arsenali alifanya mazungumzo na wasmamizi wa klabu hio ya London na inaaminika bado wanasubiri kumpiga msasa zaidi kabla ya kuteuliwa.


EmoticonEmoticon