Maneno Ya Papa Francis Kwenye Sikukuu Ya Krismas

Papa Francis
Papa Francis amekaribisha siku kuu ya Krisimasi kwa kusema kwamba Mungu anapenda kila mtu hadi wale wabaya kati yetu .
Alikuwa akizungumza na maelfu ya watu wakati wa mkesha wa siku kuu ya Krisimasi katika kanisa la St Peters Basilica mjini wa Vatican.
''Munaweza kuwa na mawazo ya finyu , unaweza kuwa umefanya mambo mabaya lakini Mungu anaendelea kukupenda'' , alisema rais huyo wa Argentina.
Matamshi yake huenda yakachukuliwa na wengi kama yale yanayolenga kashfa zinazokumba kanisa hilo , ikiwemo visa vya unyanyasaji wa kingono , kulingana na mwandishi wa BBC.
Papa Francis atarudi katika kanisa la Basilica baadaye siku ya Krisimasi ili kutoa ujumbe wa Papa wa siku ya Krisimasi duniani.
Miongoni mwa wale wanaoshiriki katika ibada hiyo ni watoto waliochaguliwa kutoka mataifa kama vile Venezuela , Iraq, na Uganda.
Mwandishi wa BBC wa Rome Mark Lowen amesema kwamba hiyo ni ishara ya wazi kutoka kwa kiongozi huyo wa kanisa lenye takriban wafuasi bilioni 1.3 kote duniani ambao huzingatia matatizo yanayowakumba wahamiaji na waathiriwa wa vita mbali na kuwafikia wale walio pembeni.
"Krismasi inatukumbusha kwamba Mungu anaendelea kutupenda sisi sote licha ya kwamba kuna waliofanya mabaya kati yetu, anasema.
''Nawapenda na nitaendelea kuwapenda kwa kuwa ninyi muna thamani kubwa mbele ya macho yangu'' , alisema kiongozi huuyo wa dini akiwa na umri wa miaka 83.
''Mungu hakupendi kwa sababu unafikiria na kufanya kile anachotaka . Anakupenda vile ulivyo. Mapenzi yake kwenu hayana masharti na hayategemei ulivyo''.
Papa pia alizungumzia kuhusu kashfa za kifedha na unyanyasaji unaokumba kanisa hilo.
''Chochote tunachokosea katika maisha yetu , chochote ambacho hakifanyiki vyema katika kanisa , matatizo yoyote yaliopo duniani hayatatumiwa kama sababu''.


EmoticonEmoticon