Meek Mill Akumbushia Tena Michano Na Mikato Yake Na Drake, Kumbe Ilikuwa Ni.....(VIDEO)

Miaka mitatu iliyopita ilikuwa ni vita kali kati ya Meek Mill na Drake, walichanana kwenye ngoma mbali mbali lakini mwaka jana waliizika bifu hiyo stejini.

Sasa Meek Mill amefunguka sababu za kuingia kwenye bifu na mkali huyo wa Canada. Kwenye mahojiano na Charlamagne Tha God, Meek Mill amesema ni vidonge vya kuondoa maumivu ambavyo alikuwa anatumia kwa wingi vilimfanya kuwa "High" na kujikuta anamtukana Drake.

"Nilikuwa nakunywa vidonge 'Percocets' 10 hadi 30 kwa siku. Unatembea na kifo. Ukiniuliza kwanini nilimvaa Drake. Siwezi hata kujua, wengi walisema ni kwasababu ya Nicki Minaj. Hapana hilo halikuwa tatizo. Walikuwa na mahusiano kabla yangu." Alisema Meek.

Charlamagne alimwambia ni kutokana na kuwa 'High' ambapo Meek alikubali ndio madawa yale yalimfanya kufanya maamuzi mabaya.

TAZAMA MAHOJIANO HAPO CHINI


EmoticonEmoticon