Mtandao Wa Twitter Kuanza Kufuta Akaunti Za Wateja Wake

Zoezi hilo linategemea kuanza kwa mtumiaji wa twitter kuokea email ambayo inakutaka kuingia kwenye akaunti yako kabla ya tarehe 11 ya mwezi wa 12 mwaka huu 2019.

Hata hivyo baada ya kupokea email hiyo na endapo mtumiaji hatoingia kwenye akaunti yake, basi akaunti hiyo itafutwa na username kuachiwa kwajili ya kutumiwa na watu wengine.
Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji huyo, akaunti hizo hazito futwa zote kwa pamoja bali itakuwa inatofautiana kwa kila mtumiaji, vilevile akaunti hizo zitafungwa miezi michache baada ya kupokea email au barua pepe yenye kutoa tahadhari juu ya kufutwa kwa akaunti yako.


EmoticonEmoticon