MUHIMU: Taarifa Mpya Toka Mtandao Wa Instagram, Tarehe Ya Kuzaliwa Na DM

Instagram kwa sasa kila mtu atakayetaka kujiunga na mtandao huo analazimika kuandika tarehe yake alisi ya kuzaliwa. 

Uamuzi wa kueleta sehemu ya kujaza tarehe ya kuzaliwa kabla ya kujiunga na mtandao huo imekuja kwa lengo la kuzuia watoto chini ya umri wa miaka 13 kutumia mtandao huo.
Hata hivyo Instagram imeainisha kuwa, kwa wale ambao tayari wanazo profile za Instagram tarehe ya kuzaliwa iliyopo kwenye kurasa ya facebook iliyo unganishwa na instagram ndio itatumika kwenye akaunti ya Instagram. 

Kwa hiyo kama ukibadilisha tarehe ya kuzaliwa kwenye ukurasa wako wa facebook moja kwa moja tarehe hiyo pia itabadilika kwenye akaunti yako ya Instagram.

Vilevile kama huja unganisha akaunti yako ya Instagram na ukurasa wako wa Facebook basi utatakiwa kuweka tarehe yako kamili ya kuzaliwa kupitia Settings kwenye akaunti yako ya Instagram. 

Kwa mujibu wa instagram, tarehe hiyo haitokuwa inaonekana na mtu yoyote sipokuwa wewe mwenyewe.
Mbali na hayo sehemu nyingine ambayo imeongezwa kwenye mtandao huo ni pamoja na sehemu mpya ya kuweza kuchagua ni nani anaweza kutuma DM. 

Kupitia sehemu hiyo mpya mtumiaji anaweza kuchagua watu aliowafuata pekee ndio waweze kutuma DM pamoja na kuwa na uwezo wa kuwekwa kwenye group na watu hao pekee.
Kama mtumiaji akiwasha sehemu hii hatoweza kuendelea kupokea DM au Direct Message kutoka kwa watu wengine isipokuwa tu watu ambao amewafuata au ame wa-follow. Sehemu hizi zote zinatagemewa kuwafikiwa watu wote siku za karibuni.


EmoticonEmoticon