Mwanamke Anahitaji Nini Kwa Mwanaume?

Katika mahusiano mwanamke anakua anahitaji mambo mbalimbali lakini si yote atakua anamwambia mpenzi wake au mume wake. 

Kichwani mwake anajua kama unampenda basi vitu hivyo hautavisahau.

Sasa hapa ndugu zangu wanaume inapasa kuchekecha akili na kujiongeza kwa maana vitu hivi huwa vinasaidia kuendelea kuwaweka karibu katika mahusiano.

Leo tutaangalia baadhi ya vitu ambavyo mwanamke/mke anavihitaji kutoka kwa mwanaume/mme wake..

1. Kutomuonesha mfumo Dume, sio lazima kwenye kila jambo basi uwe unaweka na kutanguliza mfumo dume. Siku nyingine jishushe kwa mkeo/mwanamke wako itasaidia kumvuta karibu na kuongeza mapenzi kwako.

2. Mpe sikio, hakikisha unamsikiliza mke wako anapokua anakueleza jambo. Na hapa unatakiwa umsikilize kwa makini akiwa anakueleza mambo ya msingi na mambo ya utani pia. Muda mwingine mwanamke anahitaji kusikilizwa tu roho yake inatulia.

3. Zawadi, mwanamke anapenda kupewa zawadi hivyo ni vema ukawa na utaratibu wa kumpa zawadi mke wako hata kama ni vitu vidogo vidogo kama maua, choklet, Ice cream, kutoka nae mtoko n.k

4. Mpambe kwa sifa, kwa walio kwenye mahusiano wanajua ladha ya kusifiwa na mpenzi wako. Mwanamke anahitaji umsifie kwa uzuri na mambo yake mengine. Hii ikibidi kila siku uwe unamsifia basi hauna budi kufanya hivyo.

5. Kumjulia hali mara kwa mara, mwanamke anapenda kujuliwa hali na kutafutwa mara kwa mara na mpenzi wake. Hivyo ni vema ukawa na utaratibu wa kumtafuta hata kwa kumtumia ujumbe mfupi au kumpigia hata kama upo kazini kwani haihitaji muda kumtumia mkeo ujumbe kumjulia hali. Hii itasaidia mwanamke aone unamjali na unampa kipaumbele katika maisha yako.

6. Mshukuru, uwe na utaratibu wa kumshukuru mke wako hata kwa mambo madogo madogo usisubiri mpaka afanye jambo kubwa au ukumbwe na matatizo akusaidie ndio umshukuru. Unaweza ukamshukuru kwa kukupikia, kukufulia, kulea watoto vizuri n.k

Kama nilivyoeleza hapo awali hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo mwanamke anayahitaji lakini hawezi kumwambia mwanaume ampatie…..wapo wenye uwezo wa kuwaambia wanaume wao hivyo ila kuna baadhi wanaweza kuitisha na kama umeshamzoea pia inakuwa rahisi.


EmoticonEmoticon