Mwanamke Anayetaka Kumuacha Mwanaume Huonyesha Dalili 5 Muhimu

1. Hupenda kujitenga nawe na kukaa mbali
Atakua kwenye dalili za awali za kuachana.
Tabia ya mwanamke kutopenda kukaa karibu na mumewe au mpenzi wake inatajwa kama ishara ya kuchoka au kukinai penzi.

2. Tendo la ndoa halipo kabisa
Mwanamke ambae hafurahii tendo la ndoa kwa mumewe au mpenzi wake wake yuko kwenye hatua za kuacha.
Mara zote msisimko wa kimapenzi huashiria utoshelevu wa kihisia ambao ndio unaoelezwa ni muhimu kwenye uhusiano wa kimapenzi kuliko kitu kingine.

3. Anapenda kukosoa kila kitu
Anaanza kuwa mkosoaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria. Hiyo ni ishara kuwa amekuchoka kilichobaki ni nafasi ya kuachana.

4. Hakutegemei
Mwanamke ambae ana kusudio la kukuacha huanza kwa kuondoa utegemezi, ikiwa alikua anakuomba nauli, pesa ya matumizi, ada na huduma zingine atasitisha bila bila kukuambia na bado utaona anaendelea kujimudu kama kawaida au kuteseka kimya kimya.
Kuacha kukutegemea kama zamani ni dalili za kuweza kuishi bila wewe na hivyo kutafsiri uwezekano wa kukuacha wakati wowote.
5. Anapunguza mawasiliano
Mawasiano ni bora kati ya mume na mke, endapo itatokea kwamba hakuna mawasiliano dhabiti baina yao na mpenzi wako kama ambavyo ilikua mwanza basi tambua fika penzi lenu limefika ukingoni.
Hizo ni dalili chache kati ya nyingi za mwanamke ambae anataka kuachana na wewe katika mahusiano ya mapenzi.


EmoticonEmoticon