Ni Pesa Yako Tu Itakuwezesha Kumpata Zlatan Ibrahimovic Kwa Wakati Huu

Zlatan Ibrahimovic yupo sokoni, kumpata ni pesa yako tu. Na sasa kinachoelezwa ni kwamba staa huyo huenda akawashtua wengi baada ya kudaiwa yupo njiani kwenda Everton kuungana na Kocha Carlo Ancelotti ikiwa ni bonge la dili la kijanja linalotajwa kwenda kutokea Goodison Park.

Supastaa huyo fowadi kwa sasa hana timu baada ya mkataba wake kumalizika huko LA Galaxy tangu mwishoni mwa Novemba.

Lakini, sasa anaweza kuibukia tena kwenye Ligi Kuu England kama atakubaliana na ombi la Ancelotti, anayemtaka wakapige kazi kwenye kikosi cha Everton. Ibra aliwahi kuitumikia Manchester United kwenye ligi hiyo.

Kocha Ancelotti anadaiwa amebakiza mambo machache tu kabla ya kukubali dili la kwenda kuinoa Everton kwa dili la mshahara wa Pauni 11.5 milioni kwa mwaka.


EmoticonEmoticon