Pogba Yupo Tayari Kuondoka Man U, Lampard Anaweza Kupokea Donge Nono Kupitia Hili

Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari , huku klabu ya Real Madrid ikiwa na matumaini ya kuanzisha mazungumzo ya kupunguza bei ya Man United ya £126.4m ili kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa huku akiingia miezi 12 ya mwisho katika kandarasi yake.

Kwingineko Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard anaweza kupata zaidi ya £150m kutumia baada ya marufuku ya uhamisho ya klabu hiyo kupunguzwa huku ikiwalenga winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, pamoja na beki wa kushoto wa Leicester City na Uingereza Ben Chilwell, 22..


EmoticonEmoticon