Remy Ma Afutiwa Shtaka Lililokuwa Linamkabili

Remy Ma amefutiwa shtaka la kumshambulia mwanamke mmoja aitwaye Brittany Taylor ambaye alidai rapper huyo alimpiga kwenye moja ya event mwezi April mwaka huu.

Shauri hilo lilikumbwa na ushahidi hafifu ambapo hakukuwa na video zikionesha Remy akimgusa Taylor kwa namna yoyote.

Mwanasheria wake ametoa taarifa isemayo; Shauri hilo lilimuweka pabaya mteja wake kwani alikuwa kwenye kipindi cha kujisafisha baada ya kuachiwa toka jela mwaka 2014 ambapo alifungwa miaka 6 kwa kosa la kumshambulia mtu mmoja, pia kumiliki silaha kinyume cha sheria.


EmoticonEmoticon