Simu Zitakazofutiwa Whatsapp Mwaka Kesho 2020, iPhone, Android & Windows Phones Zatajwa

Kampuni ya WhatsApp inayomilikiwa na Facebook imetoa taarifa ikisema inasikitika na uamuzi huu ila ni uamuzi wa kilazima kufanyika ili kuhakikisha wanaendelea kuwa na uwezo wa kuhakikisha watumiaji wake wanakuwa salama dhidi ya udukuzi ambao unaweza kufanywa kwenye matoleo ya nyuma ya programu endeshaji za simu.

Kwa watumiaji wa simu zenye sifa zifuatazo wajiandae kuona app ya WhatsApp ikisumbua kufanya kazi ifikapo Februari 1 2020, kama simu zao zinauwezo wa kupokea matoleo mapya ya programu endeshaji basi wanashauriwa kufanya hivyo.
Simu za iPhone 5 na 5S kutoka Apple zinaonekana kuwa ni baadhi maarufu ambazo zitaathirika kwa uamuzi huu. Bado zinatumika hasa kwa mataifa yanayoendelea. Tovuti ya DeviceAtlas ilisema kufikia mwaka huu simu za iPhone 5 na 5S zinawakilisha zaidi ya asilimia moja na nusu ya simu zinazitembelea tovuti mbalimbali mwaka huu.

·Android – Kwa android ni kwa simu zinazotumia programu endeshaji ya 2.3.3 Gingerbread na kurudi nyuma. Kama unatumia simu yeyote ya Android (mfano kutoka Samsung, Huawei, Sony na Google) iliyotoka ndani ya kipindi cha miaka 10 iliyopita utakuwa salama.

·iOS (iPhone) – Kwa simu za iPhone toleo lolote la programu endeshaji la iOS kuanzia la 8 kwenda nyuma hazitakuwa na sifa tena. iOS 8 ni programu endeshaji iliyotambulishwa mwaka 2014. Simu ya chini kabisa yenye sifa ya kupokea toleo la iOS la kisasa zaidi la iOS 8 ni simu ya iPhone 6. Hii inamaanisha kama unamiliki iPhone yeyote iliyotoka kabla ya iPhone 6 basi ujiandae app hiyo kutoweza kufanya kazi tena ifikapo Februari 1, 2020.

·Windows Phones – Simu zote zinazotumia toleo la Windows 8.1 au lolote jipya ndio wataendelea kuwa na uwezo wa kutumia WhatsApp. Matoleo ya nyuma yake haitawezekana tena.


EmoticonEmoticon