Tafiti Mpya zilizothibitishwa Juu Ya Dawa Ya Saratani

Dawa inayopunguza nusu ya hatari saratani ya matiti kwa mwanamke huendelea kufanya kazi muda mrefu hata mtu anapoacha kuitumia, wanasema watafiti.
Dawa hiyo kwa jina Anastrozole huzuwia uzalishwaji wa homoni za oestrogen, zinazochochea uvimbe wa saratani ya matiti.
Tayari dawa hiyo inatumiwa katika hospitali za umma, nchini Uingereza lakini watafiti katika Chuo Kikuu cha Queen Mary mjini London wanasema ni wanawake 10 wanao said only a tenth of eligible women were receiving it.
Watafiti wa saratani nchini Uingereza wanasema kuwa matokeo ya uchunguzi wao yalikua ni ya kuaminika.

Anastrozole inaweza kutolewa tu kwa wanawake ambao hawana uwezo wa kujifungua kwani dawa hii haiwezi kuzuwia utendaji wa homoni za uzazi oestrogen miongoni mwa wanawake wenye umri mdogo.
Tayari Anastrozole inatumiwa sasa kama tiba pale saratani ya matiti inapogunduliwa, lakini majaribio ya dawa hii yanaangazia zaidi juu ya kuzuwia saratani zinazojitokeza kwa mala ya kwanza.
Utafiti wa awali , umeonyesha kuwa anastrozole huzuwia hatari ya saratani ya matiti kwa nusu wakati wa miaka mitano anayotumia dawa hiyo mwanamke.
Lakini sasa, majaribio yaliyofanyika kwa wanawake 3,864 yanaonyesha kuwa kwa wale wanaoitumia 49% walikuwa na saratani , na hata miaka saba baadae baada ya kuitumia.


EmoticonEmoticon