Tanasha Aangukia Dili Jipya La Ubalozi Baada Ya Kujifungua

Wiki chache tu baada ya kujifungua mwana wao kwa jina, Naseeb junior, Tanasha ambaye pia ni msanii, amepata kazi mpya!
Tanasha ametuliwa balozi wa kampuni ya kitalii ya ‘Spot on vacations’.
Baada ya kutia mkataba huo, Tanasha alijitosa katika Instagram kutangaza habari hizo njema akidai kuwa “hii leo nitakuwa na habari spesheli”.
Spot on Vacations ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza katika sekta ya utalii nchini Kenya na hushughulikia maswala ya kitalii humo nchini na kimataifa kwa wale wanaotaka kujivinjari na kuzuru maeneo mbali mbali duniani.


EmoticonEmoticon