Usitumie Tangawizi Kwa Mazoea. Soma Hapa Ni Zaidi Ya Unavyofikiri

Tangawizi ni kiungo kinachotokana na mizizi ya mmea wa tangawizi.

Mmea huu unafanana na binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Kwa hapa Tanzania, hulimwa zaidi katika mikoa ya nyanda za juu kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro na kwingineko.

Mmea huu unaweza kuonekana kama wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea, lakini kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama dawa. 

Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kimekaushwa na kutengenezwa unga.

Kiungo hiki kinafaida zaidi kwa wagonjwa hasa walio athirika na ugonjwa wa Ukimwi. Hivyo, kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya maajabu ya mmea huu.

Tangawizi inaweza kukusaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza kichefuchefu, kutapika, kuharisha, kisukari, shinikizo la damu, kuongeza msukumo wa damu na kutoa sumu mwilini.

Matatizo mengine yanayoweza kuondoka kwa kunywa tangawizi ni maumivu ya tumbo na gesi tumboni.

Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia kutuliza au kuondoa kabisa mafua au flu 
Hutumika kama kituliza maumivu.

Husaidia kuboresha mmeng'enyo wa chakula tumboni.

Huthibiti shinikizo la damu.

Huboresha afya ya kinywa.

Hukinga matatizo ya ngozi hasa chunusi.

Husaidia kukuza nywele (kulinda afya ya nywele.)


EmoticonEmoticon