Wasanii Wanaoweka Album na Single Youtube Watafaidika Na Hii

Sasa Idadi ya watazamaji ambao msanii anawapata kwenye mtandao wa Youtube itamsaidia kuingia kwenye chart za album za Billboard, Waandaji wa Chart hizo kubwa duniani wametangaza kuanza kujumuisha data za mtandao wa Youtube kwenye kupanga orodha ya charts.

Kuanzia Januari 3, 2020 Data za Audio na Video za Youtube na Mitindao mingine zitaanza kutumia kwenye kupanga chart kubwa zaidi za Album 'Billboard 200' Pia data za Apple, Spotify, Tidal na Vevo zitajumuishwa kwenye mahesabu yanayozipanga album 200 bora.
Data za video zimetangazwa kuongezwa ikiwa imepita miaka 5 tangu walivyotangaza kuanza kutumia pia data za Audio kwenye kupanga chart hizo ikiwa inahashiria mabadiliko ya chart hizo kutoka kwenye mpango wa kuzingatia viwango vya mauzo (sales) hadi kuanza kuzingatia mfumo wa utumiaji (consumption model).

Data za Youtube tayari zilikuwa zinatumiwa kwenye kupanga chart za nyimbo 'Billboard Hot 100' lakini hii inakuwa mara ya kwanza kuanza kutumiwa kwenye kupanga chart za album.


EmoticonEmoticon