Afariki Baada Ya Kususia Chakula

Raia wa Marekani mwenye asili ya Misri Mustafa Kassem ameaga dunia nchini Misri baada ya kususia chakula akiwa gerezani.
Kassem mwenye umri wa miaka 54 dereva wa taxi New York, ambaye asili yake ni Misri, alikamatwa alipokuwa ameenda kutembelea nyumbani Misri 2013, alishutumiwa kwa madai ya upepelezi na kushiriki maandamano yanayopinga serikali.
Bwana Kaseem alikuwa akikanusha madai dhidi yake.
Aliacha kula chakula mwaka jana na kwa siku nne zilizopita hakuwa akinywa kinywaji chochote.
Mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Mashariki ya Kati, David Schenker, alielezea kifo cha Kassem kuwa cha kusikitisha, na ambacho kingeepukika.
Shirika la Kimataifa linalolinda haki za wafugwa wanaosubiri kuhukumiwa la Pretrial Rights International ambali lilimwakilisha, limesema kwamba aliaga dunia kwasababu ya ugonjwa wa moyo.
"Alhamisi iliyopita, aliacha kunywa kiywaji chochote na muda mfupi baada ya hapo alipelekwa katika hospitali, na kuaga dunia ," taarifa imesema hivyo.
Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa alipelekwa katika hospitali ya wafugwa kutibiwa kisukari.
"Hali yake iliendelea kudorora... na aliaga dunia Januari 13, taarifa imesema hivyo.
Mwendesha mashtaka wa Misri ameagiza mwili wake ufanyiwe uchunguzi kubaini sababu za kifo chake, shirika la habari la Misri, Mena limesema.
"Mfungwa mwengine ambaye ameuawa gerezani, "ameandika kwenye mtandao wa Twitter mwanaharakati raia wa marekani mwenye asili ya Misri Aya Hijazi, ambaye alizuiliwa kwa karibia miaka mitatu nchini Misri.


EmoticonEmoticon