AFCON Kuanza Mapema, Muda Wabadilishwa, Sio Kama Ilivyotarajiwa, Madhara Kwa Vilabu

Afcon 2021

Michuano ya mwaka 2021 ya AFCON itaanza tarehe 9 mwezi Januari baada ya tarehe hio kubadilishwa, waandalizi Cameroon wametangaza.
Kipute hicho kilipangiwa kufanyika mwezi Juni na Julai lakini ikabadilishwa kutokana na hali mbaya ya anga nchini humo wakati huo wa mwaka.
Hii ina maana kwamba huenda vilabu vya ligi ya Primia vikakosa wachezaji wa kikosi cha kwanza katika wakati muhimu wa msimu.
Mabadiliko haya yana maana kua kipute hicho hakitakinzana na kombe la dunia la vilabu litakaloandaliwa Uchina mwezi Juni mwaka ujao.


EmoticonEmoticon