Alichokiandika Cristiano Ronaldo Baada Ya Kufikisha Rekodi Kubwa Ya Wafuasi Katika Mtandao Wa Instagram

Cristiano Ronaldo Followers 200
Nyota wa klabu ya Juventus na taifa la Ureno, Cristiano Ronaldo Cristiano ndani ya rekodi nyingine mpya mtandaoni. Hii ni baada ya kuwa mtu wakwanza duniani kufikisha wafuasi (followers) millioni 200 katika mtandao wa Instagram
Official CR7 Instagram Account
Ronaldo ambaye pia anaongoza kwa kuingiza mtonyo mrefu kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa upande wa matangazo, hadi sasa ukurasa pekee ambao umemzidi kwa wafuasi (followers) Instagram, ni ukurasa rasmi wa Instagram wenyewe ambao una idadi ya 'followers' million 330+
Instagram
Ametoa shukrani za dhati kwa wafuasi wake waliokuwa naye pamoja kila siku toka anaanza safari yake ya mafanikio kupitia mtandao huo
Instagram Caption CR7
Baada ya Ronaldo anayemfatia katika orodha ni Ariana Grande, mwenye 'followers' 173.1 M, huku Dwayne “The Rock” Johnson anafatia akiwa na 'followers' millioni 170.1.


EmoticonEmoticon