Alichokisema Sadio Mane Baada Ya Kutajwa Kuwa Mchezaji Bora Wa Africa 2019

Sadio Mane
Shirikisho la soka barani Afrika wamemtaja mwanasoka bora wa mwaka kuwa ni Sadio Mane ambaye anachezea timu ya Liverpool.
Walioshiriki kinyang'anyiro cha tuzo hizo ni mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool -na wenzie walioshiriki kinyang'anyiro hicho ni mchezaji wa Misri Mohamed Salah na mchezaji wa Manchester City pamoja na winga wa Algerian Riyad Mahrez.
Mane ambaye ana umri wa miaka 27, aliweza kuisaidia Reds katika ligi ya mwaka 2018-2019 na kufunga magoli 30 katika msimu uliopita.
Aliweza kufunga magoli 15 mpaka sasa kwa mwaka 2019 mpaka 2020, na kuisaidia Liverpool kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 13.
Sadio Mane Akitoa Speech
"Nina furaha sana na ninajivunia kuwa mshindi. Kandanda ni ajira yangu ambayo ninaipenda," alisema Mane.
"Ninapenda kuwashukuru familia yangu, taifa langu , timu yangu ya taifa , wachezaji wenzangu, shirikisho na klabu ya Liverpool.Hii ni siku kubwa kwangu."
Sadio Mane Akipokea tuzo
Mane alichukua tuzo yake katika sherehe zilizofanyika huko Hurghada, Misri.
Lakini si Salah, ambaye alishinda tuzo hiyo mara mbili katika miaka miwili iliyopita wala Mahrez wali.
Mane alimaliza katika nafasi tatu za juu katika tuzo hizo katika miaka mitatu iliyopita.
Na ilikuwa ni ndoto yake kushinda tuzo hiyo ili kufikia mafanikio ya shujaa wake El Hadji Diouf, ambaye alishinda mwaka 2002.


EmoticonEmoticon