Ambaka Mbwa Mpaka Kufa, Mama Mzazi Afunguka

Mwanaume mmoja huko Kangundo Kenya katika kaunti ya machakos  amekamatwa na polisi baada ya   kufanya kitendo cha ngono na mbwa wa familia yao  hadi kumwua .Chifu wa eneo la Isinga Bethuel Kingele  amesema Boniface Wambua  mwenye umri wa makamo alipatikana na mamake akifanya kitendo hicho .

Kingele pia amesema mipira ya kondomu iliyotumiwa ilipatikana katika eneo la tukio. Hata hivyo inaripotiwa kuwa jamaa huyo hivi karibuni amekuwa akifanya vitendo visivyo vya kawaida na huenda anashawishiwa na dawa za kulevya anazotumia .

Mamake mshukiwa amesema  alishuku kulikuwa na tatizo wakati aliposkia mbwa huyo akipiga kamsa kwa muda mrefu .Mshukiwa huyo amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Kangundo  na atafikishwa kortini siku ya alhamisi . Polisi walimlazimisha mshukiwa  kumbemba mbwa huyo kama ushahidi.
Credits:Radiojambo


EmoticonEmoticon