Arsenal Wameuanza Mwaka Kwa Bashasha Chini Ya Kocha Wake Mpya Mike Arteta

Rio Ferdinand amesifu kiwango alichokionyesha Mesut Ozil na kuisaida Arsenal kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester United kwenye Uwanja wa Emirates.

Kiungo mshambuliaji alikuwa chachu ya mafanikio ya Gunners jambo lililomfanya beki wa zamani wa Manchester United kuamini Ozil sasa anafurahi maisha chini ya kocha mpya Mikel Arteta.
Arteta mwenye miaka 37, ameiongoza Arsenal kupata ushindi wake wa kwanza dhidi Manchester United ya Ole Gunnar Solskjaer.

Mwanzo mzuri wa Ozil chini ya kocha Arteta ni ishara kwamba nyota huyo atarudi katika ubora wake baada ya kuondoka kwa kocha Unai Emery.

Kwa mujibu wa Ferdinand, Ozil amekuwa mwenye furaha chini ya kocha mpya ambaye walikuwa wakicheza wote miaka mitatu iliyopita.

Ferdinand alisema: ‘Mtazame Ozil, nafikiri ni mara ya kwanza namuona akitabasabu katika miezi 18 iliyopita, na hiyo ni kwa sababu anafurahi kila kitu hata mazoezini.’

Manchester United ikicheza bila ya kiungo wake majeruhi Paul Pogba ilianza vizuri, lakini mchezo uliwabadilikia katika dakika 8, wakati Nicolas Pepe alipofunga bao kwanza likiwa ni goli lake la tano msimu huu akimalizia krosi ya Sead Kolasinac.

Bao hilo liliwafanya Arsenal kutawala mchezo huo kabla ya kupata bao la pili dakika 42, lililofungwa na Sokratis Papastathopoulos.

Vijana wa Solskajer waliingia katika mchezo huo wakiwa na rekodi ya kufungwa mechi moja kati ya tisa zilizopita walishindwa kabisa kufikia kipa wa Arsenal, Bernd Leno.
Kipigo iko kinawafanya Manchester United kubaki katika nafasi tano wakiwa nyuma kwa pointi tano kwa Chelsea ambayo ililazimishwa sare 1-1 na Brighton.

Ushindi wa Arsenal umemaliza rekodi yao mbaya ya kufungwa nyumbani katika mechi saba za mashindano yote na sasa wamepanda hadi nafasi ya 10, wakiwa nyuma kwa pointi nne kwa Manchester United.

Lakini Arsenal wapo karibu na timu zilizokuwa katika hatua ya kushuka daraja kuliko kuingia katika nne bora.
Photocredit:Gettyimages


EmoticonEmoticon