Baada Ya Future Kupata Mpenzi Wake Mpya Mwaka Huu, Imeonekana Kuwa Kuna Uwezekano Wa Kubaki Mpweke

Future and Lori Harvey
Future ni miongoni mwa watu ambao wameutendea haki usemi wa Mwaka mpya na mambo mapya, hii ni baada ya kuthibitibisha anatoka kimapenzi na Lori Harvey.

Lakini huwenda penzi hilo lisinoge sana na likaingia doa mara baada ya mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23 kushtakiwa kwa makosa mawili ya barabarani; kuwahi kugonga gari na kukimbia (Hit and Run) na pia kuweka mgomo, Kumchelewesha na kuhatarisha amani kwa Askari wa Usalama barabarani.

Kama akikutwa na hatia, basi huwenda akaenda Jela mwaka mmoja, na Future akabaki mpweke!


EmoticonEmoticon