Barcelona Yamtimua Kocha Wake Ernesto Valverde Na Kumteua...

Barcelona imemtimua kocha Ernesto Valverde na badala yake kumteua kocha wa zamani wa Real Betis Quique Setien. Valverde, 55, aliisaidia kilabu hiyo kushinda mataji mawili mfululizo ya La Liga na wanaongoza kwa tofauti ya mabao msimu huu.
Walakini, timu hiyo ya Cataln imekuwa ikiandikisha msururu wa matokeo yasiyopendeza chini ya uongozi wake na walishindwa kufikia fainali ya ligi ya mabingwa bara Uropa.
Setien, 61, alisaidia Betis kumaliza katika nambari bora zaidi kwa mara ya kwanza kutoka mwaka wa 2005 na pia kuwawezesha kufika katika nusu fainali ya kombe la Copa del Rey kabla ya kuondoka mwezi Mei.
Amekubali kutia sahihi mkataba wa miaka miwili unusu na atawasilishwa kwa vyombo vya habari hivi karibuni


EmoticonEmoticon