Bunge La Marekani Lasafisha Njia Ya Kumshtaki Raisi Donald Trump

Spika na Rais Donald Trump
Baraza la wawakilishi nchini Marekani limepiga kura kuidhinisha kutumwa kwa mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump kwenda katika Baraza la Seneti ikiwa ni hatua ambayo inaashiria kuanza kwa kesi inayoweza kumuondoa madarakani.
Hatua hiyo imekuja katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, tangu wabunge wa baraza hilo kumkuta na hatia Rais Trump ya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia juhudi za Bunge kuchunguza vitendo vyake.
Wabunge wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha azimia hilo kwa kura 228 dhidi ya 193. Huku Spika Nancy Pelosi akisaini uamuzi huo sambamba na timu ya Wabunge wa Democratic ambao wataendesha mashtaka ya kesi hiyo inayomkabili Rais Trump.
Mameneja wameteuliwa leo na spika kwa ajili ya kuendesha mashtaka kutokana na kupeleka ambacho kimepitishwa. masetena kama wazee wa baraza na baadaye kupiga kura.
Baraza hilo la Wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha upinzani cha Democrats, kutaka Rais Trump kuondolewa madarakani.
Hata hivyo Baraza la Seneti ambalo linadhibitiwa na chama tawala kinachoongozwa na Rais Trump, kitaamua aidha kumtia hatiani na kumuondoa madarakani. Jambo ambalo halitarajiwi.
Katika mkutano na wanahabari kabla ya kutia saini hati, Bibi Pelosi alisema: ''Leo tutaweka historia tutakapo peleka hati za mashtaka dhidi ya rais wa Marekani kwa vitendo vyake vya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia majukumu ya bunge kushughulikia suala hilo''.
Hati hizo kisha zikapelekwa kwenye baraza la seneti, ambapo kiongozi wake ni Mitch McConnell kutoka chama cha Republican amesema zitawasilishwa siku ya Alhamisi mchana, zoezi litakalofuatiwa na kusikilizwa kesi siku ya Jumanne ya wiki ijayo.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon