Diamond Platnumz Atumbuiza Kwenye Tuzo Za Mchezaji Bora Afrika, Mbele Ya Raisi Wa FIFA (VIDEO)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na C.E.O wa Wasafi Media Diamond Platnumz alipata nafasi ya Kuperform katika tukio la utoaji tuzo lililofanyika katika taifa la Misri.

Katika tuzo hizo mchezaji wa taifa la Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane alifanikiwa kushinda tuzo hiyo akiwashinda wachezaji Mohamed Salah anayejipiga katika klabu ya Liverpool pia na timu ya taifa ya Misri na Riyad Mahrez anayejipiga katika katika klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Algeria ingawa Maherz alishinda tuzo ya goli bora la michuano ya AFCON.
Diamond Platnumz alipata nafasi ya kutumbuiza katika tukio hilo na kuweza kuwaburudisha wageni wote waliofika katika tukio hilo ambapo wachezaji wa zamani kama Samuel Etoo nata Sadio Mane na rais wa FIFA Gianni Infantino alionyesha kufurahishwa na show hiyo ya Diamond Platnumz.

EmoticonEmoticon