Dudu Baya Afutiwa Usajili BASATA Kutojishughulisha Na Sanaa. Onyo Latolewa Kwa Watu Na Makampuni

Dudu Baya Kufungiwa BASATA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa nchini limemfutia usajili msanii Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya kutojihusisha na shughuli zozote za sanaa kuanzia leo tarehe 07/01/2020.
Barua Toka BASATA Jan.7

KISA KIZIMA
Siku ya Jana Jumatatu (Jan.6) BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) lilimtaka msanii wa Bongo Fleva, Tumaini Godfrey, maarufu Dudubaya, kufika katika ofisi za baraza hilo siku ya Jumanne Januari 7 (leo), kwa mahojiano zaidi baada ya kusambaa kipande cha video kikimuonyesha akitoa kauli zisizokuwa na maadili.
Barua Toka BASATA Jan.6
Baada ya wito huo, Dudubaya alijirekodi kipande cha video na kukirusha kwenye mtandao wa Instagram akisema:

“BASATA nimepata wito wenu na siwezi kuja, kwa sababu huwezi kuniita kuja kunionya kwa kurekodi clip za neno kufi… (tusi, kufanya ngono kinyume cha maumbile), hata mama Rwakatale kanisani huwa anasema kabisa kwamba wasagaji, walawiti wafi….(tusi)  hawataiona pepo.

“Hata katika vitabu vitakatifu Mungu hakufumba amesema kabisa kwamba walawiti wasagaji wafi…(tusi) hawataiona pepo, hata kama namfundisha mtoto wangu nitasemaje? Kufi….(tusi) ni vibaya, nimwambie kupigwa fimbo au?

“Lazima tuheshimiane, mkitaka nije lazima mhakikishe kwamba vyombo vya habari ambavyo vina ugomvi na wasanii, muweke suluhisho la amani ili muziki huu uweze kusonga mbele, siji,” alisema Dudubaya.


EmoticonEmoticon