Habari 5 Kubwa Za Michezo Alhamis Jan 23

Edinson Cavani
1.Chelsea imetoa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. 

Babake Cavani amesema nyota huyo atajiunga na Atletico Madrid ikiwa klabu hiyo ya Uhispania itaafikiana na PSG.

2. West Ham imeonesha nia ya kutaka kununua winga wa kimataifa wa Ukochi na Bournemouth Ryan Fraser, 25, ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu wa joto. Kiungo huyo pia ananyatiwa na Arsenal na Liverpool.

3. Barcelona wanajitahidi kukamilisha mkataba wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Valencia na Uhispania Rodrigo Moreno, 28, baada ya kumkosa mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30. 

4. Winga wa Uholanzi Tahith Chong, 20, yuko tayari kuondoka Manchester United mwisho wa msimu huu.

5. Klabu sita za ligi ya premia zinataka kumsaini beki wa Tottenham Muingereza Danny Rose, 29, mwezi huu.


EmoticonEmoticon