Habari 5 Kubwa Za Michezo Alhamisi Jan 30

Ivan Rakitic
1.Manchester United imefanya mwasiliano na Barcelona juu ya uwezekano wa kumsajili kiungo wa Croatia Ivan Rakitic, 31.

Pia Barcelona inaripotiwa kumnyatia mshambuliaji huyo. Kwingineko Sheffield United ndiyo klabu pekee ambayo imepeleka ofa ya usajili kwa kiungo wa klabu ya Genk na taifa la Norway Sander Berge ambaye ana thamani ya pauni milioni 27.

2. Mshambuliaji Thomas Muller, 30, ambaye anawindwa na Manchester United anaweza kuondoka Bayern Munich baada ya kukosa uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Ujerumani.

3. Mshambuliaji hatari na kinda wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Norway, Erling Braut Haaland, 19, ana kipengele cha mauzo cha pauni milioni 63 kwenye mkataba wake. 

4. Tottenham wamefanya mazungumzo na Real Madrid juu ya uhamisho wa mshambuliaji Gareth Bale, 30.

5. Mabingwa wa Uhispania Barcelona wanahangaika kutafuta streka mpya kabla ya dirisha la usajili kufungwa Ijumaa hususani baada ya Luis Suarez, 33, kupata majeraha.


EmoticonEmoticon