Habari 5 Kubwa Za Michezo IIjumaa Jan 31

Edinson Cavani
1.Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, hataihama klabu ya Paris St-Germain katika dirisha la usajili linalofungwa leo.

2. Chelsea pia wanatarajiwa kupeleka ofa ya pili ya usajili kwa mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32, baada ya ofa ya kwanza kukataliwa.

3. Kiungo mkabaji wa Serbia Nemanja Matic, 31, amegoma kuihama klabu ya Manchester United na yupo tayari kusaini mkataba mwengine wa kumbakisha Old Trafford.

4. Mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller anaweza kuihama klabu yake ya Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 30 amekuwa na klabu hiyo kwa kipindi chake chote cha uchezaji lakini kwa sasa hana raha kwa kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

5. Arsenal wanapanga kukamilisha usajili wa mkopo wa beki wa kulia wa Southampton na Ureno Cedric Soares, 28.


EmoticonEmoticon