Habari 5 Kubwa Za Michezo Ijumaa Jan 24

Carlos Tevez
1.Manchester United huenda wakamnunua mshambuliaji wao wa zamani Muargentina Carlos Tevez,35, ambaye kwa sasa anachezea Boca Juniors.
2.Chelsea wamefufua mazungumzo na Lyon kuhusu usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Moussa Dembele, 23, mwezi huu endapo watamkosa Edinson Cavani, 32 kutoka Paris St-Germain's. 
3.Liverpool wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Isco, 27, japo inadai karibu Yuro milioni 70 (£59m) kumuachilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania
4.Leicester wamekataa ofa iliyotolewa na Aston Villa kumsaini kwa mkopo Islam Slimani, 31, hadi mwisho wa msimu huu. The Foxes wanataka mkataba wa kudumu kumuachilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria, ambaye kwa sasa yuko Monaco kwa mkopo
5.Kiungo wa kati wa Real Madrid, Dani Ceballos, 23, anapania kusitisha mkataba wake wa mkopo wa msimu mzima na Arsenal kwasababu ya kukosa nafasi ya kucheza ili apate nafasi ya kujumuishwa katika kikosi cha kitaifa cha Uhispania katika michuano ya kombe la Euro mwaka 2020.


EmoticonEmoticon