Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumanne Jan 21

Christian Eriksen
1.Inter Milan wako tayari kulipa £11m na ada zingine ili kumsajili kiungo wa kati Christian Eriksen kutoka Tottenham mwezi huu.

2. Inter Milan wanakaribia kumsajili kwa mkopo beki wa Chelsea Victor Moses, 29, kujiunga na mkufunzi wake wa zamani Antonio Conte. Fenerbahce, klabu ambayo kiungo huyo wa kimataifa wa Nigeria anachezea kwa mkopo imeridhia kumuachilia.

3. Liverpool haiko tayari kumpoteza kiungo wa kati wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 28, licha ya Roma kuonesha nia ya kutaka kumnunua mwezi huu.

4. Manchester United watalazimika kulipa ada ya juu ya uhamisho kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, mwezi huu badala ya kumchukua kwa mkopo - lakini mchezaji huyo yuko tayari kuondoka PSG.

5. Mkufunzi wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anasema Gunners "ilituvunja moyo" lipoondoka Highbury na kuhamia uwanja wa Emirates. 


EmoticonEmoticon