Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumanne Jan 28

1.Kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mchezaji wa Inter Milan siku ya Jumanne baada ya kupita vipimo vya afya usiku wa Jumatatu.

2. Klabu ya Arsenal inatarajiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 30.

Pia Arsenal imebadili vigezo walivyoweka katika mkataba wa Pablo Mari, 26 baada ya ripoti ya uchunguzi wa afya yake, na kuweka wingu jeusi juu ya uhamisho huo. Usajili wa Mari umeshindikana na beki huyo yupo njini kurudi Brazil.
3. Manchester United inafikiria kumuongezea dau kiungo wa Ureno Bruno Fernandes, 25, kabla ya Ijumaa ambayo ndiyo siku ya mwisho ya dirisha la usajili.
Ingawa Fernandes amejumuishwa katika kikosi cha Sporting kitakachominyana na Maritimo Jumanne jioni, hali inayoonesha kuwa uhamisho huo unaweza kuwa mgumu kukamilika.
4. Chelsea inamfuatilia mshambuliaji wa AC Milan Krzysztof Piatek mwenye umri wa miaka 24, ambaye anawaniwa na Tottenham wakati wakijipanga kupata mbadala wa Cavani.
5. Manchester United, Arsenal na Tottenham wanavutiwa kumsajili mchezaji wa Ujerumani Emre Can mwenye umri wa miaka 26 akitokea Juventus.


EmoticonEmoticon