Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumapili Jan 26

Ole Gunnar Solskjaer Na Gareth Southgate
1.Manchester United wanaweza kumtimua kocha Ole Gunnar Solskjaer iwapo matokeo yao hayataboreka msimu huu, huku kocha timu ya taifa ya England Gareth Southgate akipigiwa upatu kumrithi Solskjaer.

2.Tottenham wanasuka mipango ya kumrejesha mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi.

3.Cavani, anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu kadhaa zikiwemo Chelsea na Manchester United. Mchezaji huyo amekubali, japo kwa mdomo tu, kuhamia klabu ya Atletico Madrid kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi.

4. Barcelona hawatarajiwi kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, na badala yake wanaelekeza nguvu zao kwa mshambuliaji wa Valencia Rodrigo Moreno, 28.

5. Tottenham na Aston Villa wamegonga mwamba kumsajili mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic baada ya timu hizo kushindwa kutoa dau la Pauni milioni 40 kwa klabu ya Fulham.


EmoticonEmoticon