Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumatano Jan 22

Quique Setien NA Luis Suarez
1.Mkufunzi wa Barcelona Quique Setien anasema kuwa klabu hiyo inamtafuta mchezaji atakayeziba pengo lililoachwa na mshambuliaji wa Uruguay aliyeumia Luis Suarez, 32 mwezi huu. 

Pia Barcelona inamtaka Pierre-Emerick Aubameyang lakini kuondoka kwake Arsenal kabla ya mkataba wake kuisha mwaka 2021 huenda kukamgharimu mshambuliaji huyo wa Gabon, 30, £15.15m.

2.Inter Miami imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 31, na David Silva, 34, ambao wataondoka klabu hiyo msimu wa joto. 

3.Manchester United imetoa ofa ya zaidi ya £30mkumnunua kiungo wa kati wa Birmingham City wa miaka 16 Jude Bellingham. 

Pia Manchester United huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 25, kwa mkataba wa £55m mwisho wa wiki hii baada ya kuafikiana na Sporting Lisbon.

4.Beki wa Real Madrid, Mhispania Alvaro Odriozola, 24, ametua Ujerumani kukamilisha uhamisho wake kwenda Bayern Munich hadi msimu utakapokamilika.

5.Fernandes aliwapuuza mashabiki wa Sporting na kusukuma kamera za televisheni baada ya kupoteza mechi dhidi ya Braga siku ya Jumanne katika kile kilionekana kuwa mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo.


EmoticonEmoticon