Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumatano Jan 29

Bruno Fernandes
1.Barcelona wamewasilisha ofa ya usajili ya dakika za majeruhi kujaribu kuipiku Manchester United kiungo wa Sporting Lisbon Portugal midfielder Bruno Fernandes, 24.
Barcelona ilipanga kumsajili Fernandes kutoka Sporting na kisha kumpeleka kwa mkopo Valencia ili kumnasa mshambuliaji wa Valencia Rodrigo,28 - lakini mazungumzo na mipango hiyo inaelekea kuanguka. 

2.Manchester United wamefikia maamuzi ya kumfanya kipaumbele chao cha usajili mwishoni mwa msimu mshambuliaji wa Valencia Maxi Gomez, 23, ambaye bei ya kuuzwa kwa mujibu wa mkataba wake ana thamani ya pauni milioni 118.5m.

3. Spurs pia wamewasiliana na Chelsea juu uwezekano wa kumsajili mshambuliji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33. (90min)Southampton wanatarajiwa leo Jumatano kukamilisha usajili wa mkopo wa beki wa Tottenham Kyle Walker-Peters, 22.

4. Arsenal haitakubali kumuuza mshambuliaji wao raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kwa dau la chini ya pauni milioni 50. Barcelona inaripotiwa kumnyatia mshambuliaji huyo.

Sheffield United ndiyo klabu pekee ambayo imepeleka ofa ya usajili kwa kiungo wa klabu ya Genk na taifa la Norway Sander Berge, 21, ambaye ana thamani ya pauni milioni 27.

5. Afisa Mtendaji Mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amegoma kusema kama wamekata tamaa ya kumsajili winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24.

Kama mbadala wa Sane, Bayern wameelekeza nguvu zao kwa kiungo wa Atletico Madrid na Ufaransa, Thomas Lemar, 24.


EmoticonEmoticon