Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumatatu Jan 20

Jose Mourinho
1.Antonio Conte amemshutumu Jose Mourinho kwa kubadilisha maneno yake baada ya mkufunzi huyo wa Spurs kumkosoa mwenzake wa Inter kwa kuzungumzia kuhusu mchezaji wake Eriksen.

2. Maombi ya Manchester City na Barcelona ya kutaka kumsajili beki wa kati wa Inter Milan Alessandro Bastoni, 20, yamekataliwa.

3. Bruno Fernandes, 25, ameambia Sporting Lisbon anataka kujiunga na Man United na mazungumzo zaidi yamepangwa wiki hii baada ya kugonga mwamba kuhusu thamani ya mchezaji huyo wa Portugal.

4. Inter Milan pia ina hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Croatia Luca Modric , 34, kutoka Real Madrid.

5. Arsenal itajaribu kumsaini beki wa Bayern Munich na Ujerumani Jerome Boateng, 31, kwa mkopo mwezi Januari kabla ya kuwasilisha ombi la £50m ili kumnunua beki wa kati wa Ufaransa na klabu ya RB Leipzig Dayot Upamecano, 21, mwisho wa msimu.


EmoticonEmoticon