Habari 5 Muhimu Za Michezo Alhamisi Jan 16


1.Klabu ya Inter Milan imeafikiana makubaliano binafsi na kiungo wa Denmark Christian Eriksen,27, ili wamsajili moja kwa moja lakini klabu yake ya Tottenham inaitaka Milan kuongeza dau lao mpaka Euro milioni 10.

2.Barcelona wanakaribia kumsajili kiungo wa Brazil Matheus Fernandes, 21, kutoka klabu ya Palmeiras kwa dau la Euro milioni 7, lakini pia kuna uwezekano wa euro milioni 4 kuongezeka.

3. PSG imeitaka Atletico Madrid kupandisha dau lao la usajili ili kumnasa nyota wa Uruguay Edinson Cavani kutoka Euro mioni 10 mpaka 30. Mshambuliaji huyo anamaliza mkataba wake na PSG mwishoni mwa msimu huu.

4. Arsenal wanapanga kutoa pauni milioni sita ili kumnasa beki wa kushoto wa wa PSG Mfaransa Layvin Kurzawa, 27, kabla ya mchezaji huyo kumaliza mkataba wake na PSG mwishoni mwa msimu. 

5. West Ham wanasuka mipango ya kumsajili kwa mkopo kiungo wa Chelsea Ross Barkley 26. Mchezaji huyo alishawahi kuhudumu chini ya kocha mpya wa West Ham David Moyes katika klabu ya Everton.


EmoticonEmoticon