Habari 5 Kubwa Za Michezo Jumamosi Jan 18

1. Mshambuiaji wa England na Tottenham anayeuguza jeraha Harry Kane, 26, huenda akarejea katika mazoezi mepesi katika kipindi cha wiki tisa hivi na kwamba anatarajiwa kuanza kuichezea Tottenham kufikia katikati ya mwezi Aprili.

2.Manchester United inakaribia kufikia makubaliano na Sporting Lisbon kumsaini kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandes , 25 katika mkataba unaoweza kuwa na thamani ya £60m lakini uhamisho huo hautafanyika kwa haraka.

3. Inter Milan inakaribia kumsaini winga wa Chelsea Victor Moses, 29, baada ya mkufunzi Antonio Conte kuwasilisha ombi maalum kwa klabu hiyo ili kumsaini mchezaji huyo wa Nigeria, ambaye kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Uturuki Fenerbahce. 

4. Klabu ya Los Angeles Galaxy imemsaini mshambuliaji Javier "Chicharito" Hernandez, 31, kutoka Sevilla kwa kandarasi itakayomfayan mchezaji hyo kuwa mchezaji anayelipwa kitita kikubwa zaidi katika ligi hiyo ya soka nchini Marekani.

5. Beki wa kushoto wa Paris St-Germain Layvin Kurzawa, 27, ametoa ishara kwamba anakaribia kujiunga na Arsenal mwezi huu baada ya kutangaza kwamba amejiunga na ajenti mmoja wa Uingereza. agency. 


EmoticonEmoticon