Hatma Ya Bruno Fernandes Kuelekea Manchester United, Dau Lake Latajwa

Bruno Fernandes
Manchester United wamekubaliana mkataba wa kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes kutoka Sporting Lisbon.
United watalipa kitita cha kwanza cha takriban Uro milioni 55 kwa mchezaji huyo wa miaka 25, ingawaje marupurupu huenda yakafanya kitita hicho kufikia Uro milioni 80.
Uhamisho wa Fernandes utakamilika baada ya uchunguzi wa kimatibabu na masuala mengine ya kibinafsi. Vilabu hivyo vimekua vikijadiliana wakati wote wa dirisha la uhamisho huku makubaliano yakiafikiwa Jumanne.


EmoticonEmoticon