Huyu Ndiye Msanii Pekee Wa Afrika Aliyepata Nafasi Ya Kutumbuiza Coachella 2020

Mwaka huu Jukwaa la Coachella limepata bahati ya kubarikiwa na Mwafrika mmoja tu, ni DJ Black Coffee toka Afrika Kusini.
Dj Black Coffee
DJ huyo maarufu ametajwa kwenye orodha ya wasanii kibao ambao wataungana na Travis Scott, Frank Ocean na Rage Against the Machine waliotajwa kama Vinara wa tamasha hilo kwa mwaka 2020.

Hii ni mara ya tatu kwa Black Coffee kutumbuiza kwenye Coachella, tamasha linaloteka hisia za watu wengi duniani. Alifanya hivyo mwaka 2016, na tena akaalikwa mwaka 2018 ambapo 'Set' yake ilitawaliwa na playlist ya kumuenzi rafiki yake kipenzi marehemu Avicii.
Mwaka Jana Afrika iliwakilishwa na wakali wa Nigeria, Burna Boy na Mr. Eazi pekee. Mwaka huu limetajwa kufanyika Wikendi za April 10-12 na April 17-19.


EmoticonEmoticon