Huyu Ndiye Mtu Muhimu Aliyerudisha Penzi La Travis Scott Na Kylie Jenner - PICHA

Travis Scott, Kylie Jenner, Stormi
Mtoto ni kiungo muhimu sana katika familia, hii imedhihirika baada ya mtoto wa Travis Scott na Kylie Jenner, Stormi kuchochoe penzi la wazazi wake kurudi kama zamani baada ya mwaka jana kuripotiwa kuachana.
Katika picha iliyopigwa na mtandao wa TMZ imewaonyesha wawili wao wakiwa pamoja na mtoto wao Stormi katika maeneo ya Magic Kingdom mjini Orlando huku taarifa za ndani zikidai kuwa penzi limerudi Kama kawaida baada ya mtoto wao Stormi kuwa akimuulizia Baba yake mara kwa mara pindi awapo na Mama yake.


EmoticonEmoticon