
Huu ni ugonjwa ambao hutokana na kula chakula au kunywa
kinywaji ambacho kina sumukuvu aina ya aflatoxin.
Sumu hii husababishwa na ukungu (fangasi) ambao
hutokana na hali ya unyevunyevu wakati wa mazao yakiwa shambani,
wakati wa kuhifadhi, usindikaji au wakati wa kusaga.
Vyakula ambavyo hushambuliwa na sumu hii ni kama;
1. Nafaka kama vile mahindi, mtama na uwele.
2. Mbegu za mafuta kama vile karanga.
3. Mazao mengine ni kama korosho na mihogo.
Madhara ambayo
hutokea baada ya ulaji wa vyakula vyenye sumukuvu kwa kiwango kikubwa yanaweza
kuwa ya muda mfupi au mrefu.
Madhara
ya muda mfupi yanaweza kuwa;
Tumbo
kujaa maji
Mapafu
kujaa maji
Na wakati
mwingine kupoteza maisha.
Madhara
ya muda mrefu yanaweza kuwa;
-Saratani
ya ini.
-Figo
kushinxwa kufanya kazi.
-Kinga ya
mwili kupungua
-Kudumaa
kukua kwa watoto.
-Kupoteza
maisha
Jinsi ya
kujikinga na ugonjwa wa sumukuvu;
1. Kausha
mazao kikamilifu baada ya kuvuna kabla ya kuyahifadhi.
2. Fuata
ushauri wa wataalam wa kilimo juu ya uhifadhi wa vyakula.
3.
Usihifadhi vyakula vilivyotobolewa na wadudu.
4. Kula
vyakula aina tofauti tofauti.
5.
Hakikisha nafaka hazinyeshewi na mvua baada ya kuvunwa.
6.
Dhibiti wadudu waharibifu wa mazao baada ya kuvunwa.
7.
Unashauriwa kukoboa nafaka kama vile mahindi ili kupunguza kiasi cha sumukuvu
wakati wa mlipuko.
8.
Teketeza mbegu zilizoharibika au kubadilika rangi wakati na baada ya kuvuna.
9.
Kwa kuwa sumu hii haiishi hata kwa kupika, epuka kabisa kutumia vyakula
vyenye ukungu.
10. Ghala
la kuhifadhia chakula linatakiwa liwe na mzunguko wa hewa ya kutosha.
Vuna mazao shambani mapema baada ya kukomaa kabla ya ukungu kujitokeza. Kisha anika mazao juani kwenye turubai, mikeka au vichanja mpaka yakauke vizuri na kuyahifadhi vyema sehemu isiyokuwa na unyevu ili kuzuia fangasi au sumu aina ya aflatoxin
EmoticonEmoticon