Kauli Ya Kocha Mpya Wa Barcelona Dhidi Ya Messi Yaibua Utata, Yajadiliwa

Hivi karibuni kumekuwa na msemo ambao umeibuka kuwa katika hii dunia muogope sana Mungu na Teknolojia na pengine kauli hii ya kocha mpya wa Barcelona, Quique Setien inatudhihirishia hilo baada ya mwaka jana 2019 kabla hata haijajulikana kuwa atakuja kuwa mwalimu wa Muargentina huyo akisema siku ambayo Messi atatundika daluga kunako soka basi atalia milele.

Kauli hii iliyoishi mpaka sasa imeibuka upya kwenye mitandao na kupewa uzito mkubwa hasa baada ya yeye kutangazwa rasmi kuwa kocha wa Barcelona ambayo Messi yupo chini yake kwa sasa akiwa kama mwalimu.
Siku zote, Quique Setien amekuwa akivutiwa na soka la Messi hata kabla hajajua kuwa siku moja atakuja kubeba mikoba ndani ya Barcelona.

“Siku ambayo Messi atatundika daluga, nitalia milele. Hakuna mtu mwingine kama Messi , nilishapata bahati ya kuona wachezaji wengi wazuri lakini hawakuwa na muendelezo mzuri na kudumu kwa miaka 12 au 14 ndani ya ubora ule ule.”

“Naamini hakuna mchezaji na sifahamu kama Pele katika muda wake alidumu kwenye ubora wake kwa muda mrfefu kama Messi ndani ya miaka 12.”
“Sifahamu zaidi idadi ya ‘hat-trick’ ambazo amefunga. Ni furaha kumuona akijumuishwa kikosini na kumuangalia kila siku ya Jumapili ndani ya miaka yake hii 12 ama 14.
“Kitu ambacho nakipenda kwa Messi ni kwamba siku zote amekuwa bora na amezidi kudhihirisha hilo kila wikiend.”
Maneno hayo ya kocha Quique Setien aliyasema baada ya Barcelona kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Betis huku Messi akitupia mabao matatu kwenye mechi hiyo mwaka 2019.
Quique Setien alitangazwa kuwa kocha mpya wa Barcelona kwa mkataba wa miaka miwili na nusu akichukua mikoba ya Ernesto Valverde aliyetimuliwa kazi mapema wiki hii.


EmoticonEmoticon