Kauli Za Donald Trump Kuhusiana Na Iran

Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Iran "inaonekana kurudi nyuma"baada ya kufyatua makombora dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq.
Bw.Trump, alisema kuwa hakuna raia wa Iraq au Marekani aliyeuawa katika shambulio hilo japo kambi hizo ziliharibiwa kidogo.
Kambi za kijeshi za Irbil na Al Asad zilishambuliwa mapema Jumatano alfajiri.
Iran ilisema ilichukua hatua hiyo kulipiza kisasi mauaji ya wiki iliyopita ya jenerali wake wa ngazi ya juu Qasem Soleimani.
Ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani ililenga msafara wake akiwa na maafisa wa wakuu wa kundi la waasi wanaoungwa mkono na Iran,mjini Baghdad katika hatua ambayo ilizorotesha uhusiano kati ya Iran na Marekani.
Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Khamenei amesema shambulio hilo lilikuwa "kofi la usoni" kwa Marekani na kutoa wito kwa nchi hiyo kuondoka mashariki ya kati.
Shambulio dhidi ya Soleimani pia liliwaua wanachama wa kundi la waasi wanaounga mkono Iran ambao pia wamesema watalipiza kisasi.
Hata hivyo, makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amekimbia kituo cha habari cha CBS kwamba "ujaususi" unaashiria kuwa Iran imewaambia waaasi hao ambao ni washirika wake wasishambulie ngome zozote za Marekani.
"Tunapokea taarifa za ujasusi za kutia moyo kwamba Iran inatuma ujumbe kwa baadhi ya waasi kutoshambulia ngome za Marekani ama raia, na tunatarajia wataendelea kutoa ujumbe huo," Bw Pence aliambia kituo hicho.

Kauli Za Donald Trump
 "Hakuna Mmarekani yeyote aliyejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na utawala wa Iran, usiku wa kuamkia jana ," alisema.
"Iran inaonekana kurudi nyuma, hatua ambayo ni nzuri kwa pande zote husika," aliongeza.
Pia alisema kwamba "Marekani ina uwezo mkubwa kijeshi na kiuchumi, hali ambayo inaifanya kuheshimika". "Japo tuna zana za kijeshi za kisasa na zilizo na uwezo mkubwa wa kivita, haimaanishi lazima tuzitumie."

Bw. Trump pia alisema Marekani itawekea vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Iran, hadi "itakapobadili tabia yake".
"Iran lazima iachane na azma yake ya nyuklia na kukomesha ufadhili dhidi ya ugaidi," alisema.
"Ulimwengu uliostaaarabika lazima utume ujumbe wa pamoja kwa utawala wa Iran. Kampeini yenu ya ugaidi, mauaji na ghasia haitakubaliwa tena na mtu yeyote. Haitakubaliwa kuendelea mbele."


EmoticonEmoticon