Kibarua Cha Ole Gunnar Solskjaer Chanukia Nyasi

Ole Gunnar Solskjaer
Kinachosemwa kwa sasa ni kuhusu usalama wa kibarua cha Kocha Ole Gunnar Solskjaer huko Manchester United, chochote kinaweza kutokea muda wowote.

Mashabiki wa Man United wamekuwa waki-piga kelele wakitaka kocha huyo afutwe kazi baada ya timu kushindwa kufanya vizuri hasa baada ya kuku-mbana na kipigo cha mabao 3-1 uwanjani Old Trafford kwenye nusu fainali ya Kombe la Ligi.

Matokeo hayo ya-liripotiwa kuwakera pia Sir Alex Ferguson na bosi kubwa Ed Woodward jambo lililowafanya watu kuanza kumhesabia siku kocha huyo za kubaki Man United.
Alijitutumua na kuwachapa 4-0 Norwich City kwenye mchezo uliofuatia katika Ligi Kuu England, lakini hilo bado halijamwacha Ole salama.

Tayari kwa sasa imeshaanza kufuatiliwa Man United itahitaji kulipa fidia kiasi gani itakapoamua kumfuta kazi Solskjaer katika mkataba wake kufikia mwisho na imeelezwa ni pesa ndogo kuliko iliyowahi kulipwa fidia kwa makocha waliomtangulia walipofun-guliwa mlango wa kutokea huko Old Trafford.
Ole Gunnar Solskjaer
Fidia ya kuvunja mkataba wa Ole inaripotiwa ni Pauni 5 milioni tu. Lakini, kama Man United wataamua kumfuta kazi Solskjaer ndani ya wiki chache zijazo basi jambo hilo litawafanya kufikisha Pauni 40 milioni walizotu-mia kulipa fidia makocha iliyowatibua. Makocha waliofungashiwa virago na wababe hao ni Jose Mourin-ho, Loius Van Gaal na David Moyes.
Photoscredit:gettyimages


EmoticonEmoticon